AZAM FC YAIBUKA NA USHINDI 1-0 DHIDI YA TIMU YA LIPULI FC YA ILINGA. - smart ago
728*90

Breaking

Sunday, 24 September 2017

AZAM FC YAIBUKA NA USHINDI 1-0 DHIDI YA TIMU YA LIPULI FC YA ILINGA.


     Klabu ya Azam baada ya kuifunga Lipuli kwa bao moja lililofungwa na Mbaraka Yusuph, limeiwezesha timu hiyo kusogea mpaka nafasi ya pili kuwa na pointi 10 sawa na Mtibwa.
Katika kipindi cha Usajili klabu hiyo iliondokewa na wachezaji wao wengi nyota, Aish Manula, Erasto Nyoni, John Bocco waliotimkia Simba hali ambayo ilianza kuzaa sintofahamu kwa mashabiki wa timu hiyo na kujiuliza nini kitatotekea.
Kocha wa timu hiyo, Aristica Cioaba ameonekana kuja kivingine zaidi baada ya kutumia mfumo wa 3-5-2 kwa kuwachezesha mabeki watatu na kujaza viungo wengi hali ambayo inakuwa inasumbua timu nyingi zinazokutana na Azam.
Lipuli licha ya kuwakamata Yanga katika nafasi ya viungo waliocheza kwenye Dimba la Uhuru, walishindwa kutawala dhidi ya Azam baada ya Mromania wa Azam kumjazia viungo wenye uzoefu wa hali ya juu.
Lipuli walikuwa wanacheza mpira mwingi na kuanzisha mashambulizi, lakini walikuwa wamemsimamisha Lambele Jerome ambaye alionekana kushindwa kutamba mbele ya Daniel Amoah,Yahya Mohammed na Aggrey Morris ambao kadri siku zinavyozidi kwenda mbele wameonekana kuwa vizuri na kutoruhusu mabao.
Aristica Cioaba alikuwa akimtumia Bruce Kangwa kupeleka mashambulizi kwa upande wa kushoto, huku upande wa kulia akicheza Himid Mao tofauti na ilivyozoeleka kwani alikuwa akicheza kama kiungo mshambuliaji anayetokea pembeni na alifanikiwa kutoa pasi ya bao kwa Mbaraka Yusuph.
Lipuli licha ya kupoteza mchezo dhidi ya azam, tinu hii bado inaonekana wachezaji wazoefu walio katika timu hiyo wanapambana kuisaidia timu kufanya vizuri tofauti na timu inayotokea ukanda wao ‘Njombe Mji’ ilivyo hivi sasa.
Kwa mwendo ambao wanaenda nao Azam hivi sasa kuna vitu vingi vinakuja mbeleni, wachezaji wao wana umoja na kutaka kupata matokeo katika kila mechi na kuonyesha kuwa hakuna mapengo yoyote yaliyotokea baada ya kuondokewa na baadhi ya wachezaji.

No comments:

Post a Comment