Fanya hivi ili kuitunza komputa/laptop yako ili kuepuka kuharibika. - smart ago
728*90

Breaking

Sunday, 29 October 2017

Fanya hivi ili kuitunza komputa/laptop yako ili kuepuka kuharibika.

         Fanya haya mara kwa mara itakusaidia namna ya kuifanya laptop yako kutokuharibika unapoitumia.
  • Update mara kwa mara
  • Tumia Antivirus iliyokuwa inayokuwa updated angalau kila siku. Ku update hakuchukui muda mrefu kama una update kila siku huchukua hata dakika kadhaa tu. Ninashauri anti-virus hii ya AVG Free Antivirus kwani ni bora sana.
  • Zima computer yako kwa kufuata njia mahususi na sio kuchomoa tu nyaya au kuzima ukutani.
  • Kwa laptop pindi inapokuwa imetumika kwa muda mrefu na ikachemka sana jaribu kuizima/sleep/hibernate kwa muda ili ipoe hivyo utasaidia kuifanya iwe na kasi zaidi.
  • Dumisha nguvu na uimara wa betri kama unatumia laptop. 
  • Pia epuka sana kuweka laptop yako karibu na maji au unyevu wowote ili kueouka kuharibika na kuzima kwa ghafla.
  • Epuka kuinstall programs ambazo huzitambui kazi zake ambazo hizo zinaweza kuwa threats ya laptop yako au kuifanya kuwa nzito wakati wa kuload file au program husika.
  • Epuka kuinstall window mara kwa mara kwa kila tatizo unalokumbana nalo, kumbuka sio kila tatizo la laptop yako au komputa yeyote linatibika kwa kuweka window hapana na ondoa dhana hiyo kwani unaweza kuifanya laptop yako isiwe safe mood.  Tafadhali mpendwa mgeni, je,ungependa kujua zaidi kuhusu kifaa gani na jinsi ya kukitunza ili kiweze kuwa na manufaa zaidi kwako. Usisite kinitaarifu nami nitaandaa post kwa ajili yako kwani wewe ni mtu muhimu sana. 
           Asante kwa kusoma hii. karibu tena katika blog iliyo kwa ajiri yako ya smarta ago. asante sana na karibu tena.

No comments:

Post a Comment