Kama kawaida karibu tena katika blog ya smart ago ili kuweza kupata elimu mbalimbali ndani ya kipengele hiki cha Afya na lengo ni kutaka tunufaike katika maisha haya tunayoishi na si kuhangaika karibu sana na mualike na mungine asanteni sana.
Kwa kawaida watu wengi wamekuwa wakipata matatizo mbalimbali pasipo wao kutambua nini suluhisho la magonjwa yao lakini mungu hakutuumba kwa bahati mbaya wala hakuumba vitu kama hivi yaani mimea tofautitofauti kwa bahati mbaya hivyo kwa anaetambua ndiye ataweza kuiona faida ya kutumia mimea tofautitofauti. karibu na soma hapa chini faida hizo za kitunguu swaumu,
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Namna ya kuandaa na kutumia kitunguu swaumu fanya haya yafuatayo bila kukosea chochote kama ilivyo hapo.
1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
4. Menya punje moja baada ya nyingine
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10.
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa yafuatayo, soma hadi mwisho kwa umakini.
Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:
- Huondoa sumu mwilini
- Husafisha tumbo
- Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
- Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
- Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
- Huzuia kuhara damu (Dysentery)
- Huondoa Gesi tumboni
- Hutibu msokoto wa tumbo
- Hutibu Typhoid
- Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
- Hutibu mafua na malaria
- Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
- Hutibu kipindupindu
- Hutibu upele
- Huvunjavunja mawe katika figo
- Hutibu mba kichwani
- Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
- Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
- Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
- Hutibu maumivu ya kichwa
- Hutibu kizunguzungu
- Hutibu shinikizo la juu la damu
- Huzuia saratani/kansa
- Hutibu maumivu ya jongo/gout
- Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
- Huongeza hamu ya kula
- Huzuia damu kuganda
- Husaidia kutibu kisukari
- Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
- Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
- Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
- Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
- Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
- Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
soma hapa madhara ya kitunguu swaumu kwa umakini.
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
- Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
- Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
- Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
- Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
- Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
- Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.
Fanya hivyo na uone faida yake, karibuni tena katika blog yangu ya smart ago na mungu awabaliki sana kwa ushauli au mapendekezo weka comment yako hapo chini tutayajenga kama kawaida. asante
YAANI MIMI NIMEKUNYWA JANA USIKU PUNJE MOJA NA LEO ASUBUHI PUNJE 2 SIO KWA KUHARISHA HUKO
ReplyDelete