Wanawake watatu wamemtuhumu rais
Donald Trump, kwamba aliwafanyia ukatili wa kijinsia miaka iliyopita
kabla hajawa rais wakitaka baraza la Congress kumchunguza trump
kutokana na kashfa hizo.
Wanawake walioibua kashfa hiyo dhidi ya
Rais Trump ni Jessica Leeds, Samantha Holvey, na Rachel Crooks wamesema
kuwa rais Trump bila ridhaa yao alikuwa akiwashika shika, kuwabusu kwa
nguvu na ukatili mwingine.Lakini hata hivyo ikulu ya white house imesema kuwa madai ya wanawake hao si ya kweli.
"Rais alikwisha elezea wazi wazi kashfa hizi, katika mikutano yake ya kampeni hata kabla hajawa rais. Na tunaamini kuwa madai haya yalikwisha jibiwa kwa mfumo huo."Sarah Huckabee Sanders.
Rachel Crooks katika madai yake dhidi ya kashfa hiyo ya rais Trump, anasema kuwa yeye alilazimishwa kupigwa busu na rais Trump, nje ya lift ya majengo ya ghorofa za Trump enzi hizo akiwa na miaka 22.
Japo kuwa mkasa huo ulitokea miaka mingi iliyopita, anasema bado Trump anapaswa kuchukuliwa hatua.
Mwanamke mwingine anayemtuhumu rais Trump ni mlimbwende wa mwaka 2006 Bi Samantha Holvey, ambaye anasema ,Trump alihudhuria mashindano hayo na alikuwa anawakagua mwilini kama vile nyama inavyokaguliwa buchani, na amesema kuwa hana nia ya kumchukulia hatua rais Trump bali anaweka wazi kile alichofanyiwa.
Rais Trump tangu aingie madarakani amekuwa akiandamwa na kashfa mbali mbali zikiwemo za kisiasa na zile zinahusiswa na biashara zake.
No comments:
Post a Comment