Karibuni tena katika blog ya smart ago, kazi yangu mimi ni kuhakikisha nakuandalia vitu vizuri kwenu wasomaji na watembeleaji wa blog hii pendwa karibuni sana. leo nazungumzia kwa namna ipi unaweza kuishi na mpenzi au mke/mme wako pasipo kukwazana.
Mara nyingi tumekuwa tukisikia na kuona mahusiano ya watu hayadumu kwa muda mrefu kwa wapendanao hii yote ni kwa sababu ya kutotambua namna ya kuishi na wapenzi wetu. sasa ili uweze kuishi na mpenzi wako vyema fanya haya yafuatayo-
1.Tambua mwenzako anapenda nini.
Hapa tunagusia tabia na mienendo katika mahusiano maana yake ni lazima ujue kwanza tabia yake ni ipi na huwa anapenda nini hasa katika maisha yake ili usije kuhisi kuwa hayuko nawe labda anakudanganya badala yake unakimbilia kumuacha. mfano mwenzako anapenda kupiga stori na watu wote hasa jinsia tofauti alafu wewe ukimuona unapatwa na hasira hata huwezi kuvumilia unachukua maamuzi yasiyo bora kwake, kumbuka (A good fighter never angry)
2.Usiwe na wivu uliopindukia kwake.
Ni kweli katika mahusiano lazima uwe na wivu na mpenzi wako lakini angalia usije ukafikia hatua ambayo sio nzuri kwa wivu wako, uwe na self control katika mahusiano yako kwani kama ni wako itabaki kuwa wako tu. jaribu kuona yote anayofanya mpenzi wako ni ya kawaida ata kama unahisi jambo furani kabla ya maamuzi kaa chini na yeye mwambie kinachokusibu tena kwa sauti na sura ya tabasamu atakuelewa kuliko wewe kupaniki na kuanza kumtupia maneno machafu atakuona kama una mzuzua akiri kwani kile ulichomsemea yeye kwake anaona ni uongo hivyo ataanza kuwa na hofu akidhani kuwa unamtafutia sababu ya kumuacha na kuanza kujiandaa kwa lolote na hapo ndiyo mahusiano yanaanza kuingia utatani, hivyo tuwe makini sana.
3.Kuwa mvumilivu kwa hali yeyote kwa mpenzi wako.
Unapoamua kuwa katiaka mahusiano unapaswa kuwa mvumilivu kwa mpenzi wako kwa lolote lile hata kama iweje we umvumilie tu kumbuka unampenda na hukulazimishwa kumpenda hivyo hata kama amekosea mara ngapi yakupasa msameheane na mgange maisha mapya ili mahusiano yadumu na hapa inaweza kuwa ni kushuka kwa kipato, kupokea taarifa mbaya inayomuhusu mpenzi wako, na mengine mengi kwa kwa namna yake ni lazima kuwa mvumilivu kwa yote.
4.Uwe na tabia ya kuomba na kupokea msamaha kwa mpenzi wako.
Hapa tunapaswa kuwa katika mfumo mzuri wa kuomba msamaha kwa mpenzio unapoona tu umemkosea na kama umekosewa pia inakupasa uwe tayari kupokea msamaha mara mpenzi wako akuombapo msamaha usisite na ufanye hivyo kutoka moyoni.
5.Epuka kuwa na maamuzi mabaya ya ghafla kwa mpenzi wako.
Hapa nazungumzia yale maamuzi ambayo anayafanya mtu ghafla kwa mpenzi wake tena maamuzi hayo yanaweza kuwa ni hatari kwake na mwenzake pia. mfano umeona mpenzi wako kafanya ndivyo sivyo unaamua ghafla kumuacha na kumpigia au kumtext sms za kumtusi na kumuacha bila kuwaza na kufikiri mara mbili hadi zaidi juu ya kutatua tatizo hilo, hivyo ushauri wangu tuwe wasitahimilivu katika mahusiano, mapenzi bila vikwazo sio mapenzi ila mkipita katika vikwazo na kuvivuka ndiyo kukomaa kwa mapenzi.
6.Kumpa haki zote mpenzi wako zinazomfaa.
Hapa kwa ufupi kila mmoja anatambua namna ya kumfanyia mpenzi wake yote yanayofaa katika maisha ya mahusiano, upendo wa kweli ndio kitu bora ambapo ndani yake unapata vitu vingi na vizuri vinavyoweza kukuza na kudumisha mahusiano yenu kama vile heshima,nidhamu,mapenzi ya kweli, na mengine mengi yanayompendendeza mpenzi wako pasipo vikwazo vyovyote.
kwa ufupi hayo ni mambo baadhi ambayo ukiyatimiza kwa uadilifu basi hutokuwa kama wale wanaolia katika mahusiano yao.
Asanteni kwa kutembelea blog yangu ya smart ago kumbuka kumualika mungne ili tuweze kuchangia mawazo kwa pamoja ili tusonge mbele kwa kupeana ujuzi katika kupata elimu iliyo bora na kwa lolote lile koment hapo chini tutasaidiana. asante karibuni tena na tena
No comments:
Post a Comment