KIKOSI cha Simba, Alhamisi kilijitanua kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu
Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Singida United
katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Katika mchezo huo ambao Simba ilikuwa ikihitaji zaidi matokeo ya ushindi
ili ijihakikishie nafasi yake ya kukaa kileleni, ilifanikiwa kupata bao
la mapema dakika ya tatu lililofungwa na Shiza Kichuya. Beki wa kati wa
timu hiyo,
Asante Kwasi, aliongeza bao la pili dakika ya 24 baada ya kukwepa mtego wa kuotea aliowekewa na mabeki wa Singida United.
Mara baada ya Kwasi kufunga bao hilo, kocha mpya wa Simba, Pierre
Lechantre raia wa Ufaransa, alinyanyuka kwenye kiti chake akiwa jukwaani
na kuanza kushangilia pamoja na ofisa habari wa timu hiyo, Haji Manara
huku akiwapungia mkono mashabiki wa timu hiyo.
Dakika ya 65 wakati Emmanuel Okwi wa Simba anajiandaa kuingia kuchukua
nafasi Mzamiru Yasin, mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakimshangilia kwa
nguvu jambo ambalo lilimhamasisha straika huyo na kuipatia Simba bao la
tatu dakika ya 75.
Okwi aliongeza bao la nne dakika ya 82 ambapo kwa mara nyingine,
Mfaransa, Lechantre aliinuka kwenye kiti na kushangilia kwa nguvu.
Katika mchezo huo, Simba ilifanya mabadiliko ya wachezaji wawili ambapo
ilianza kumtoa Mwinyi Kazimoto dakika ya 22 na nafasi yake kuchukuliwa
na Said Ndemla kabla ya dakika ya 65 kutoka Mzamiru na kuingia Okwi.
Kwa upande wa Singida United, dakika ya 59 ilimtoa Kiggy Makasi na
nafasi yake kuchukuliwa na Salum Chuku. Kwa matokeo hayo, Simba
inaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 29
ikifuatiwa na Azam yenye pointi 27. Mtibwa Sugar ni ya tatu ina pointi
24, Singida inakamata nafasi ya nne na pointi 23, huku Yanga ikiwa ya
tano na pointi 22.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Smart Ago ni jina la blog yangu ambapo blog hii nimeianzisha kwa sababu nyingi na tofautitofauti.Ambapo miongoni mwa malengo yangu ni kuwaandalia na kuwafikishia habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi,michezo,siasa na kutoa elimu nyingine nyingi katika jamii yangu inayonizunguka ili kuweza kuwa urahisi wa wao kutohangaika kutafuta semina pengine wengine wako vijijini ata kuangalia runinga kwao ni ngumu hivyo watapata habari kwa kuandika smartago.blogspot.com popote walipo kwa kutumia simu zao za smartphone, karibuni sana na mualike na mwenzako.
No comments:
Post a Comment