Kumetokea kuandikiana kwenye mtandao wa Instagram baada ya Mwimbaji Mkongwe Ray C kuandika na kusema hajapendezwa na kitendo cha Nandy kuimba copy ya nyimbo za Ray C kwenye Tamasha la Fiesta.
Baada ya Ray C kumuonya Nandy asiendelee tena kuimba hizo nyimbo, Nandy nae alimjibu kwa hekima na kusema kuwa hakuwa na nia mbaya na amekua akifanya hivyo kuwaenzi Wakongwe ambao ndio wamewafungulia njia.
Ray c kupitia IG account yake aliandika hivi "Jamaani hii tabia sio nzuri kabisa!!! Sijafa bado! Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye show zenu muwe mnaniitaga basi!sina cancer ya koo ya Kushindwa kuziimba hizo nyimbo!Nandy hii mara ya mwisho ukipanda fanya kazi zako! Hii mara ya pili ujue! Mashabiki zangu hamuwatendei haki!i don't like it sipendi! Maana hata tukigongana muda mwingine hata salam hamnipi kwahiyo staki mazoea.......
"Niliimba tusitaftiane visa tena Pisha sio tena Presha"
Nandy nae akamjibu hiviii "Dadaangu Ray c, kama wote tulivyosema kabla ya kuimba juzi, mimi ni mmoja wa wasanii wanaokukubali kama mmoja wa wasanii waliotufungulia njia ya muziki wetu ulipo. Sitaacha kukuheshimu na kukubali kwa hilo wewe na wengine wengi tu. Siamini kukusifia na kukuenzi ni lizima uwe umekufa hapana siamini kwenye hilo sis nafanya jambo hili zuri kwa moyo wangu mzuri kama ulivyomuenzi Mama Mwanahela kwa nyimbo zake ulizorekodi za mahaba ya dhati na nimezama. Heshima yangu kimuziki kwako itabaki siku zote kama nilivo imba nyimbo za wengine nyimbo zao kama mwasiti, king kiki, yemi alade na recho".
No comments:
Post a Comment