Klabu ya Everton imemfuta kazi meneja Ronald Koeman baada ya kichapo cha 5-2 Jumapili kutoka kwa wakali wake Arsenal kuwaacha wakiwa kwenye eneo la kushushwa daraja kwenye jedwali Ligi ya Premia.
Taarifa ya klabu hiyo imemshukuru Ronald kwa huduma alizotoa kwa klabu hiyo katika kipindi cha miezi 16 iliyopita.
Everton wamo nafasi ya 18 Ligi Kuu England na wameshinda mechi mbili pekee kati ya tisa walizocheza ligini msimu huu.
"Bado naamini ninaweza kubadili hali hii," Koeman alikuwa amesema Jumapili.
Koeman amekuwa meneja wa tatu Ligi ya Premia kufutwa msimu huu baada ya Frank de Boerwa Crystal Palace na Craig Shakespeare wa Leicester.
No comments:
Post a Comment