WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Halmashauri na Mji wa
Bunda pamoja na Madiwani washirikiane katika utekelezaji wa ujenzi wa
miradi ya maendeleo.
Pia amewaagiza watumishi wa umma katika halmashauri ya wilaya na mji wa
Bunda wafanye kazi kwa bidii na wawahudumie wananchi bila ya ubaguzi wa
aina yoyote.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Ijumaa, Januari 19, 2018) wakati
akizungumza na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya na wa
Halmashauri Mji wa Bunda, katika ukumbi wa Halmashauri ya Bunda.
“Watumishi wa umma acheni kukaa sana maofisini tengeni muda wa
kuwatembelea wananchi katika maeneo yao na shirikianneni nao katika
kutatua kero zinazowakabili. Madiwani na watumishi lazima mshirikiane
ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema watumishi na madiwani wakishirikiana katika usimamizi wa
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, wilaya itafanikiwa
katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Pia Waziri Mkuu aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa mujibu wa
sheria na taratibu za utumishi na wajiepushe na vitendo vya rushwa,
wizi , ufisadi na uzembe kwa sababu vinarudisha nyuma maendeleo ya
wananchi.
Awali, Waziri Mkuu alikagua mradi wa maji wa Bunda na baadae alizindua
kikundi cha Ushirika cha Igembe Sabo na kukagua skimu ya umwagiliaji wa
zao la mpunga ya Nyatwali wilayani Bunda.
Waziri Mkuu alihitimisha ziara yake wilayani Bunda kwa kuhutubia mkutano
wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Stendi Mpya katika mji mdogo wa
Bunda.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Smart Ago ni jina la blog yangu ambapo blog hii nimeianzisha kwa sababu nyingi na tofautitofauti.Ambapo miongoni mwa malengo yangu ni kuwaandalia na kuwafikishia habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi,michezo,siasa na kutoa elimu nyingine nyingi katika jamii yangu inayonizunguka ili kuweza kuwa urahisi wa wao kutohangaika kutafuta semina pengine wengine wako vijijini ata kuangalia runinga kwao ni ngumu hivyo watapata habari kwa kuandika smartago.blogspot.com popote walipo kwa kutumia simu zao za smartphone, karibuni sana na mualike na mwenzako.
No comments:
Post a Comment